Tundu Lissu akifutwa machozi wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo, ni halali.
Mbunge wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge. Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Mosses Mzuna wa Makahama Kuu Kanda ya Moshi alisema ushahidi uliotolea na upande wa walalamikaji, umeshindwa kuthibitisha kuwa, walalamikiwa walivunja au kiuka sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki, hoja zote 11 zilizoletwa na walalamikaji, zimeonyesha ushahidi wa kuhisi,kusikia na kushuku, ambao hauna uhalisia wa mambo.