Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao waliooa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001.
Baadhi ya Watanzania waliokimbilia jijini Mogadishu nchini Somalia mwaka 2001 wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar. Wa kwanza ni Mohammed Adam (38) akiwa amembeba mwanae mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili wakitokea Mogadishu Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za kibinadamu.
Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Zanzibar.(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar).