Mke: Vipi mume wangu mbona umewahi kurudi na una majonzi?
Mume: Wenzangu wote ofisini wamefariki umetokea moto ghafla
Mke : Mungu wangu we umeponaje?
Mume: Tumbo lilikuwa linanisumbua naharisha, nikawa nimekwenda choo cha ofisi ya jirani, kile cha ofisi yetu kibovu, ndio kilichoniponesha
Mke: Nazionea huruma familia za wenzio sasa wataishije?
Mume: Nimesikia kuwa Bima itailipa kila familia ya marehemu milioni 20
Mke: Dah!! Unaona mambo yako ya kuharisha harisha umeikosesha familia yako milioni ishirini hivi hivi.
0 Comments