Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, Hawa Ghasia ( aliyesimama) akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya s awali ‘ Orientation ‘ kwa Wakurugenzi hao wapya 36 kati ya 45 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ( hawapo pichani) Augosti 13, mwaka huu, ( kushoto ) ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, na ( kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Alphayo Kidata, mafunzo hayo ni ya siku nne.
Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wapya wa Halmashauri za Wilaya , wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, Hawa Ghasia ( hayupo pichani) Augosti 13, 2012, wakati alipofungua mafunzo ya siku nne ya awali ‘ Orientation ‘ kwa Wakurugenzi hao wapya wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wapatao 36 kati ya 45.
Wakurugenzi Watendaji wapya wa Halmashauri za Wilaya , wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia , ( wanne kutoka kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Joel Bendera ( watatu kutoka kushoto) na kushoto kwa Waziri ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Lydia Mbiaji , mara baada ya Waziri huyo kufungua mafunzo ya awali ‘ Orientation ‘ ya siku nne kwa Wakurugenzi hao wapya 36 kati ya 45 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.Picha zote na John Nditi.
0 Comments