Muda mchache uliopita
tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho
Ngassa ambaye klabu yake Azam leo imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya
Simba.
Katika mazungumzo hayo
Mrisho Ngassa amesema kwamba yeye binafsi hajapata taarifa rasmi kutoka kwa
klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba. "Kiukweli hizo taarifa mie
nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti lakini muajiri wangu bado hajanipa
taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia huu utaratibu sidhani kama ni sahihi,
wanawezaje kuniuza timu nyingine bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu
katika hiyo timu nyingine nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa
kuamini kama Azam watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba
Ngassa tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au
kukataa.
Ngassa akaendelea
alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa kuna hali ya
kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na mshabiki wa klabu hiyo
ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote nilichokaa pale. Unaweza
ukajiuliza kwanini mimi mpaka leo kwanini mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi
kwangu au ninakuwa na ukaribu nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa
baraka zote na klabu yangu, yaani niliondoka vizuri. Azam walikuja wakaongea na
Yanga wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa
chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje leo wao wameshindwa
kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa kuninunua kutoka Yanga.
Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba ingebidi na mie nipewe taarifa ili
kuweza kukubaliana mahitaji yangu binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini
sivyo walivyofanya."
Alipoulizwa kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo. Taratibu lazima zifuatwe na kuniuza kama kiroba cha mchele, kwa hali ilivyo mpaka sasa sitoweza kujiunga na Simba"
By Aidan Charlie
0 Comments