Mr & Mrs Eddy ambao kwa jana waliweza kutufuturisha waungwana wote wa kijijini kwetu..Allah atawalipa kwa wema na ukarimu wa siku ya jana.
Baadhi ya kina mama wakichukua chakula tayari kwa kufutar hapo jana...wallah kila mmoja alifurahia madikodiko.
Baba mwenye nyumba Mr Eddy akiwa na baadhi ya watoto waliokusanyika katika kufutar pamoja nyumbani kwa Mr Eddy.
Baadhi ya wakina baba waliohudhuria wito wa kufuturu pamoja nyumbani kwa Mr Eddy.
Baadhi ya kina mama wakiendelea kupata maakuli na vinywaji hapo jana nyumbani kwa shoga yao mama Denzil(Mrs Eddy).
Baadhi ya mabinti wadogo nao walikuwepo kupata futar ya pamoja nyumbani kwa Eddy kijijini kwetu hapo jana.
Kwa upande wa kija baba nao waliitika wito wa kujumuika pamoja na kufutar kwa pamoja hapo jana nyumbani kwa bwana Eddy.
Ndugu yetu kipenzi na mwalimu wa watoto wetu kijijini kwetu kuhusu suala zima la mambo ya madrassa naye alihudhuria futar ya pamoja nyumbani kwa bwana Eddy hapo jana.
Kama ilivyo kawaida kwamba kila lenye mwanzo huwa na mwisho,pichani ni mama Denzel ambaye ni mama mwenye nyumba (mrs Eddy) aki`smile kama shukrani kwa kila mmoja aliyepokea wito wa kufutar pamoja kwenye nyumba yao hapo jana.
Maganga One Blog na Majembe yake yote yaliyofika kufutar pamoja hapo jana tunashukuru sana kwa sadat ya Mr & Mrs Eddy hapo jana na Allah atawalipa kwa wema wenu.