Mabondia Maneno Osward "Mtambo wa Gongo" (kushoto) na Rashidi Matumla "Snake Boy" wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao utakaofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Dar live jijini Dar es Salaam.
Promota wa mchezo wa masumbwi,Kaike Siraju katikati akiwainua mikono juu mabondia Maneno Osward kushoto na Rashidi Matumla wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Dar Live,Mbagala jijini Dar es Salaam .