Nyota wa Kikapu, Tyson Chandler Mchezaji mahiri wa kikapu toka Marekani anayechezea timu ya New York Knicks kama "center" na pia anachezea timu ya Taifa ya Marekani yuko jijini Dar Es Salaam kwa ziara maalumu.

Tyson yumo kwenye timu ya Taifa ya Marekani iliyotwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya 2012 yaliyomalizika London na alicheza michezo yote.

Tyson ambaye msimu huu wa ligi ya NBA iliyoisha alichaguliwa kuwa mchazaji bora mzuaji/Mlinzi (NBA Defensive Player of the year) pia ni balozi wa heshima wa UNICEF.

Katika ziara ya Dar amefanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo/ watoto wa mitaani katika viwanja vya Don Bosco.

Tunamshukuru sana Tyson na pia tunawashukuru UNICEF kwa ushirikiano wao. Pichani anaonekana Tyson akiwa Don Bosco wakati wa mafunzo kwa vijana wadogo/watoto wa mitaani na picha nyingine ni Mkurugenzi wa Michezo na Ushirikiano wa UNICEF USA akiwa na Magesa/TBF-VP.

Phares MagesaMakamu wa Rais,Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF).