Polisi wa Ugiriki wamewakamata watu karibu 5,000, kwenye operesheni dhidi ya
wahamiaji haramu, huku kukiwa na wasi-wasi kuwa wakimbizi kutoka Mashariki ya
Kati, wanaweza kutaka kuingia kwa sababu ya vita vya Syria.
Watu zaidi ya 1,000 wamekamatwa hadi sasa, na wengine zaidi wanatarajiwa
kuzuwiliwa.
Wahamiaji wasiokuwa na nyaraka zinazofaa watarejeshwa makwao.
Zaidi ya 80% ya wahamiaji wanaoingai Umoja wa Ulaya, wanapitia Ugiriki.
Na baadhi ya wanasiasa wameitaka serikali ichukue msimamo mkali kuhusu
wahamiaji haramu, wakati Ugiriki inapita kwenye msuko-suko mkubwa kabisa wa
kiuchumi kwa miongo kadha.
0 Comments