Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete katika Hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali ya kuchangisha fedha kwa Wanawake Wajasiriamali ikiwa ni Kipindi cha Mwezi wa Wanawake Wajasiriamali nchini wenye Kauli mbiu "Msichana Amka Ujasiriamali ni Ajira" ambapo amewataka Wakinamama waliokwisha fanikiwa kuwaongoza Wasichana na wajasiriamali wanaochipukia njia sahihi za kibiashara zitakazowawezesha kufikia mafanikio katika biashara na kutumia ubunifu wao kama rasilimali

Mjasiriamali na Mkufunzi Bi.Namsifu Nyagabona akishirikishana uzoefu wa Biashara na wanawake wajasiriamali katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali iliyohudhuriwa na Wabunge Wanawake pamoja na Wake za Viongozi uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam

 Meza kuu ikisikiliza Shuhuda za Kinamama waliofanikiwa katika Biashara za Ujasiriamali. Mgeni rasmi katika hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasirimali Mama Asha Bilal (wa tatu kulia), Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda( wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA Bi. Hulda Kibacha (kulia), Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Therezya Huvisa (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Taasisi ya MOWE Bi. Elihaika Mrema (wa tatu kushoto)
Baadhi ya Wake za Viongozi, Wabunge Wanawake na Wanawake Wajasiriamalia waliohudhuria hafla ya Usiku wa Mwanamke Mjasiriamali iliyofanyika jijini Dar es Salaam Serena Hotel