Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa tatu kutoka kushoto), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kushoto), Mhe. Hussein Kattanga na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kulia), Mhe. Ignas Kitusi wakiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wapya walioteuliwa kushika nyadhifa hizo katika Mikoa ya Iringa, Tabora na Mara, (mwenye tai nyekundu) ni Mhe. Juma Kasairo ameteuliwa kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Iringa, kushoto kwa Mhe Kasairo ni Mhe. Issa Hassan Magori ameteuliwa kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mkoa wa Tabora na kushoto kwa Mtendaji Mkuu ni Mhe. Faisal Abubakari Kahamba ambaye ameteuliwa kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Mara.
Mhe Jaji Mkuu amewakabidhi hati za uteuzi ofisini kwake jana (Picha na Mary Gwera)