YANGA jana imefanikiwa kuibuka na pointi tatu baada ya kuilaza Toto African kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Mabao ya Yanga yamefungwa na Didier Kavumbagu (Dakika ya 2), Mbuyu Twite (Dakika ya 21) na Jerryson Tegete (Dakika ya 69).