Wanamgambo waliojihami kwa bunduki, wamekalia bunge la Libya,
kuelezea masikitiko yao kuhusiana na jinsi serikali mpya ya nchi hiyo
ilivyoundwa.
Wanamgambo hao wanataka baadhi ya mawaziri kuondolewa, kwa sababu
wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na rais wa zamani wa nchi hiyo Muammar
Gaddafi.
Malori kadhaa, yakiwa yamesheheni silaha za kutungulia ndege zimejipanga nje
ya bunge la nchi hiyo.
Libya iliandaa uchaguzi wa amani mwezi Julai mwaka huu, na wanasiasa wa nchi
hiyo waliafikiana kuhusu jinsi ya kubuni serikali mpya siku ya Jumatano.
Waziri Mkuu Ali Zidan alipataa uungwaji mkono kutoka kwa bunge la nchi hiyo
kuhusiana na jinsi alivyowachagua mawaziri wake.
Waziri huyo mkuu aliwateuwa wanasiasa wasioegemea upande wowote na wenye
misimamo ya kadri, katika baraza lake ili serikali yake ya mseto ikubalike na
pande zote.
Lakini mazungumzo hayo yalivurugwa na maandamano mapema wiki hii na siku ya
Jumatano, watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, walivamia bunge la nchi hiyo na
wamekuwa wakilidhibiti tangu wakati huo. |
0 Comments