Stori: Mwaija Salum na Joan Lema
KUTOKANA na ndoa
hiyo kuwa ya aina yake, hivi karibuni waandishi wetu walimuweka kati Bob
Junior na kumbana kwa maswali ya “why, kwanini, ikawaje” aoe
kimyakimya wakati yeye ndiye ‘prezidaa’ wa masharobaro? Bob Junior akafunguka: “Nilifunga ndoa Desemba mwaka jana. Nililazimika
kuoa kimyakimya kutokana na masharti ya wazazi wa pande zote mbili
kwamba ndoa isifungwe kwa mbwembwe.”
Alisema, hata idadi ya
wahudhuriaji katika ndoa hiyo ilidhibitiwa, hivyo kuruhusu ndugu na
marafiki wachache kushuhudia tukio hilo.
“Kikubwa ni kufunga ndoa inayompendeza Mungu ili atupe Baraka zake na tuishi katika maisha yanayompendeza.
“Kwa Watanzania, napenda wajue tu ukweli kwamba nimeoa na mke wangu
anatarajiwa kujifungua hivi karibuni,” alisema Bob Junior a.k.a Mr.
Chocolate.
0 Comments