Na Haruni Sanchawa
MUDA mfupi baada ya msanii, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuachiwa kwa dhamana, mama mzazi wa staa huyo, Lucresia Kalugila alipagawa na kumsahau mwigizaji Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye alikuwa mstari wa mbele kusimamia kesi ya mwanaye.Tukio hilo lilitokea juzi Jumatatu katika Mahakama Kuu, Dar wakati nyota huyo alipokuwa akipokea majibu ya ombi la dhamana. Mara baada ya Mahakama kutamka kuwa dhamana ilikuwa wazi, mama Lulu alichanganyikiwa kwa furaha na kutimka bila kumuaga Dk. Cheni.
“Mama yaani umenisahau mara hii umeondoka hata bila kuniaga?” alihoji Dk. Cheni ambapo mama huyo alimuomba msamaha kwa kuwa haikuwa dhamira yake.