Wapiganaji wa kiisilamu nchini
Somalia wanasema kuwa mwanajeshi wa pili wa Ufaransa amefariki kutokana
na majeraha yake baada ya jaribio la kumuokoa kukosa kufanikiwa.
Msemaji wa wanamgambo wa al-Shabab ameelezea
kuwa komando huyo alifariki kutokana na majeraha ya risasi na kwamba
mwili wake na ule wa mwenzake itaonyeshwa baadaye.![]() |
| Wanamgambo wa Al Shabaab wlaifurushwa mjini Mogadishu kufuatia harakati za jeshi la AU |
Hata hivyo wanamgambo wanasema kuwa yungali hai wakati wakiamua cha kumfanyia.
Msemaji wa Al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab, aliambia vyombo vya habari kuwa: ''Komando wa pili alifariki kutokana na majeraha yake. Tutaonyesha miili hiyo kwa Ufaransa''
Siku ya Jumamosi , rais Francois Hollande alisema kuwa wanajeshi hao wawili walitolewa kama kafara katika operesheni hiyo na kwamba bwana Allex aliuawa na wanamgambo waliokuwa wamemteka.
Makabiliano yalianza kati ya al-Shabab na makomando hao baada ya wao kuvamia mji wa Bulo Marer siku ya Ijumaa na Jumamosi.
Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian alisema kuwa wanamgambo 17 wa Al Shabaab wameuawa.
Uvamizi ulijiri saa chache baada ya wanajeshi wa Ufaransa kuingilia kati hali nchini Mali.


0 Comments