Jean-Marie Runiga
Waasi wadai kutaka kuimarisha hali ya maisha
Waasi hao ambao wanaongozwa na Bosco Ntaganda, ambaye anasakwa na
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ICC, kwa madai ya uhalifu wa
kivita, wamepiga hatua kubwa tangu mwaka uliopita.
Waasi hao waliuteka mji wa Goma, mwezi Novemba lakini walijiondoa kufuatia shinikizo za kimataifa.
Kiongozi wa shughuli za kisiasa wa waasi hao,
Jean-Marie Runiga, aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali ya
Congo, haikuwa imetimiza mapendekezo yake ya kusitisha mapigano na kuwa
wanajeshi wa serikali wamekuwa wakijiandaa kuwashambulia.
Kundi hilo la M23 limeshutumiwa na Umoja wa
mataifa kwa kufanya maasi dhidi ya raia jambo ambalo kiongozi wake Jean
Marie Runiga amekanusha.
M23 imesema iataka kuimarisha hali ya maisha ya
watu wa Mashariki mwa Congo, lakini Umoja wa Mataifa umedai kuwa waasi
hao wanaungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda, madai ambayo
yamekanusha vikali za serikali hizo mbili. |
0 Comments