Wapiganaji wa kiisilamu wameuteka mji uliokuwa
unadhibitiwa na wanajeshi wa serikali licha ya harakati za kijeshi dhidi
ya wapiganaji hao kwa usaidizi wa Ufaransa.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian
alisema kuwa mji wa Diabaly, ambao uko umbali wa kilomita 400 kutoka mji
mkuu ulitekwa katika makabiliano yaliyofanyika kati ya wapiganaji hao
na wanjeshi Jumatatu.
Bwana Le Drian alisisitiza kuwa harakati za jeshi la Ufaransa zimeweza kupiga hatua.
Aliongeza kuwa wapiganaji hao waliweza kutoroka
na kukimbilia Mashariki mwa nchi lakini akakiri kuwa wanjeshi wa
Ufaransa wanakumbwa na wakti mgumu kukabiliana na waasi ambao ambao
wamejihami vilivyo.
Awali waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa,
Laurent Fabius alisema kuwa harakati za jeshi la Ufaransa katika
kusaidia wanajeshi wa Mali dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu hazitachukua
muda mrefu sana.
Juhudi zao zitadumu tu wiki chache.
Mnamo Jumapili, Jeshi la wanahewa la Ufaransa
liliimarisha mashambulio yake dhidi ya wapiganaji hao hasa kwenye miji
ya Gao na Kidal.
Wizara ya Ulinzi ya ufaransa inasema mashambulizi hayo yatakamilika katika muda wa wiki kadhaa.
Mamia ya wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika Magharibi wanatarajiwa
kujiunga na wanajeshi wa Ufaransa. Tayari Uingereza imetoa ndege mbili
za kijeshi kusaidia katika usafirishaji wa wanajeshi na vifaa nchini
mali.
Jeshi la Ufaransa lmekuwa likipambana na
wapiganaji hao tangu Ijumaa , wakisaidia wanajeshi wa serikali kutwa
maeneo yaliyotekwa na wapiganaji hao na hata kufanikiwa kutwa mji wa
Konna.
Ufaransa imeitisha mkutano na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, baadaye hii leo.
Akiwahutubia waandishi wa habari,bwana Fabius
alikataa kikosi kushirikishwa kwa muda mrefu kama ilivyo nchini
Afghanistan chini ya NATO.
''Baadaye tutaweza kuondoka lakini hatuna nia ya kukaa hapa kwa muda mrefu.''
Bwana Fabius alisema kuwa ikiwa Ufaransa
isingeingilia mgogoro huu, kulikuwa na tisho la wazi kuwa wapiganaji hao
wangeweza kuingia zaidi ndani ya Mali na hata kufika mji mkuu Bamako,
huku athari kubwa zikijitokeza.
|
0 Comments