Stori:Johannesburg, Afrika kusini
MSHIRIKI anayewakilisha Bongo katika Shindano la Big Brother 2013 ‘The Chase’, Ammy Nando ameanza kashkash baada ya kamera kummulika akijivinjari na mshiriki wa Namibia, Dilish.
Ammy Nando
Mpango mzima ulijiri Mei 29, mwaka huu, usiku wa tatu katika Jumba la Big Brother na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa katika pozi za kimahaba kuoneshana upendo (romantic time).
Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao, Mtanzania Ammy Nando alijiachia kwenye bafu moja na kuoga na mrembo huyo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.

DILISH
Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uzuri wa Dillish unaweza kumvuta na mambo yakawa kama ilivyotokea kwa Mwisho Mwampamba na Merly Shikwambwane mwaka 2011.
Kwa upande mwingine mshiriki kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe alipata nafasi ya kuzungumza na Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu awali kudata kwa Huddah.