Wenye nyuso za furaha ni Mr n` Mrs Yusuf wakipata flash baada ya shughuli za dua kumalizika.
Mama mwenye nyumba ambaye leo alikuwa na ugeni mzito toka mataifa mbalimbali..hapa akiwakaribisha baadhi ya wageni na kuwaelezea mawili matatu.
Ndugu,jamaa na marafiki waliohudhuria shughuli za dua nyumbani kwa Yusuf leo hii
Wageni toka sehemu mbalimbali nao pia walikuwepo..pichani ndugu Ally Nahimana akitoa mawili matatu.
Kutoka kushoto ni mzee wetu mzee Balles,anayefuata ni mzee wetu mzee Mossi na kaka yetu Rachid wakibadilishana mawazo baada ya dua kumalizika.
           Bidada Azza Yusuf kushoto na mama yetu Mrs Balles au mama Sarah
Baada ya dua shughuli ya uchomaji wa nyama iliendelea na watu walivunja mifupa kwa sana tu.Pichani Eddy na ndugu Samir hawakujiharibia katika sector ya Nyama choma.
Kama kawaida baada ya dua Sadaka ilichukua nafasi yake...pichani kina mama wakipata sadaka.
                     Sadaka ikiendelea kutolewa kwa upande wa kina mama
Kutoka kushoto ni Mrs Maganga One na Mrs Eddy a.k.a Fatma Mashauzi Classic wakila pozi la ufoto...shughuli inaendelea na mafoto kibaoo ni hapo baadae.