Wafuasi wa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi
Wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed
Morsi wamefanya maandamano makubwa mjini Cairo, huku waumini wa dini ya Kiislamu
wakiadhimsiha Ijumaa ya kwanza tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Wafuasi wa kiongozi huyo wa vugu vugu la Muslim Brotherhood walijikusanya
Mashariki mwa mji huo, kushinikiza utawala wa kijeshi kumrejesha madarakani
kiongozi wao.
Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo
akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir.
Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood
huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi
wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa.
Marekani kutuma ndege za kivita Misri
Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri,
kusitisha harakati zake za kuwakamata wanachama wa vuguvugu la Muslim
Brotherhood na kuonya dhidi ya kulenga kundi lolote.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon vile vile ameonya utawala huo wa
Misri kutotenga chama chochote cha kisiasa katika harakati za kutatua mzozo wa
kisiasa unaokumba taifa hilo.
Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney amesema, utawala wa
Washington hauamini kuwa ni lazima isitishe misaada yake ya Misri.
Marekani inatarajiwa kupeleka ndege nne za kivita aina ya F-16 nchini Misri,
lakini haijathibitisha kuwa msaada huo utatolewa lini.
Serikali ya Marekani imesema, inachunguza ikiwa aumuzi huo wa jeshi la Misri
kumuondoa madarakani rais Morsi ni mapinduzi ya Kijeshi kwa kuwa sheria za
Marekani inazuia serikali kutoa misaada kwa nchi yoyote ambayo kiongozi
aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ataondolewa kupitia mapinduzi.
Wafuasi wa rais Morsi wamekuwa wakiandamana wiki nzima karibu na kambi ya
kijeshi iliyoko Mashariki mwa mji mkuu wa Cairo, ambako wanaamini kuwa kiongozi
wao anazuiliwa na maafisa wa kijeshi tangu alipoondolewa madarakani. |
0 Comments