Kikundi cha viongozi wa dini nchini Syria kimetoa Fatwa
inayowaruhusu watu wanaoishi katika vitongoji vya mji mkuu Damscus vinavyokumbwa
na vita kula nyama ambayo kwa kawaida huwa imeharamishwa
Kwenye kanda ya video, viongozi hao walisema kuwa watu wanaokumbwa na njaa
wanaweza kula nyama ya Paka,Mbwa na Punda.
Fatwa hiyo imetolewa huku kukiwa na ripoti za watu kukumbwa na njaa katika
kitongoji cha Muadhamiya mjini Damsacus moja ya vitongoji vilivyotekwa na
waasi
Mashirika ya misaada yameitaka serikali kuruhusu misaada ya kibinadamu
kupelekwa katika eneo hilo , ambako wenyeji wamekwama.
Mamia ya raia , hata hivyo walifanikiwa kutoroka maeneo hayo mwishoni mwa
wiki baada ya vita kusitishwa kwa muda.
Katika ujumbe wao wakati wa sherehe za Eid al-Adha viongozi wa kidini
waliwashauri wenyeji wa eneo la Ghouta kula nyama ambazo kwa kaiwada huwa
haziliwi katika dini ya kiisilamu.
Viongozi hao walisema huu ni wito kwa dunia nzima na kuongeza kuwa ikiwa hali
itaendelea ilivyo, watu wanalio hai watalazimika kula wafu.
Sio mara ya kwa fatwa kama hii kutolewa kwenye mzozo wa Syria.
Fatwa sawa na hii iliwahi kutolewa mjini Homs na Aleppo wakati mapigano
yalikuwa mabaya zaidi katika miji hiyo.
Mashirika ya misaada ambayo yamekuwa yakitoa msaada wa chakula katika maeneo
ya vita yamesema kuwa lazima jambo hilo liwe muhimu kama ilivyo kuharibu silaha
za kemikali za Syria. |
0 Comments