Rehema Fabian.
MAMA WA MTOTO ATAOLEWA? Hata hivyo, Diamond alisema mwanamke atakayemzalia mtoto siyo lazima ndiye awe mke wake wa ndoa kwa sababu suala la ndoa ni jingine na kuzaa ni jingine.
“Wangapi wanazaa na wanaheshimiana bila kufunga ndoa? Suala la ndoa ni kubwa, siyo la kukurupukia. Inawezekana mwanamke akanizalia na akiwa na tabia ninazopenda akawa mke wangu lakini inawezekana tukaishia kuzaa tu.
“Kifupi suala la ndoa ni mipango. Ikiwa sawa basi nitaoa lakini kwa sasa ninachozungumzia ndugu yangu ni kupata mtoto, baaasi!” alisisitiza Diamond.
WALIOPITA KWA DIAMOND Diamond amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wasichana kadhaa, kati yao wengine walikubali na wengine walikana uhusiano huo huku baadhi mapenzi yakiwa ya siri.
Baadhi ya wasichana waliowahi kuwa penzini na Diamond ni pamoja na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Rehema Fabian, Jokate Mwegelo, Pendo Mushi na Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambaye mpaka sasa yuko mikononi mwake.
Wema wakati penzi lao likiwa motomoto, ilisemekana ana ujauzito lakini ghafla ikawa kimya, ilikuwaje? Diamond anafafanua: “Alisema ilitoka, sasa ningefanyaje? Lakini pia sipendi kuzungumzia sana mambo hayo yaliyopita. Tuongee kuhusu yajayo.”
Kuhusu mimba ya Penny? Huyu hapa Diamond: “Ni kweli aliwahi kusema kuwa ana mimba yangu lakini baadaye alisema imeharibika. Siwezi kusema zaidi ya hapo.”
KUTOKA RISASI Kila mmoja ana uhuru wa kupanga na kuamua maisha aliyoyachagua. Wazo la kuwa na mtoto ni zuri lakini ni vyema Diamond akawa makini ili kiu yake hiyo isije ikazima ndoto zake katika maisha.
|
0 Comments