DAUDI BABU MRINDOKO ARUDISHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM LEO TAREHE 18/07/2015. NURU MPYA YA MABADILIKO KATIKA UMMA-MOSHI MJINI UMOJA NI USHINDI Kijana Daudi Babu Mrindoko aliyeshawishiwa kugombea ubunge na wakazi wa Moshi Mjini,merudisha Fomu Leo tarehe 18/07/2015 saa 10:00 jioni na kupokelewa na Katibu wa Chama CCM Wilaya ya Moshi mjini -Ndugu.Loth Ole-Nesele. Wananchi wa jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro mwanzoni mwa mwaka 2015 walianza kumshawishi kijana Daudi Babu Mrindoko  kuchukua fomu za kugombea ubunge wa jimbo la Moshi-Mjini,Wananchi jimboni Moshi-Mjini wanaamini kabisa kuwa pendekezo lao la mgombea Daudi Mrindoko ndio funguo pekee ya kumaliza matatizo na ndio funguo ya kuelekea kwenye nuru mpya ya maendeleo jimboni. 
Pendekezo hilo la wananchi wa Moshi Mjini kijana Daudi Mrindoko ambaye ndiye mgombea mwenye umri mdogo kuliko wote jimboni humo ambaye amelelewa na CCM kuanzia Chipukizi hadi UVCCM na sasa anaelekea kuwania nafasi ya kuwatumikia ubunge mjini Moshi na kauli yao mbiu wananchi hao ni "Nuru Mpya ya Mabadiliko katika Umma " Vipaumbele-Uchumi, Afya,Elimu, Hifadhi ya jamii(Yatima, Wajane na Wazee) Daudi Babu Mrindoko 2015-2020