Wiki iliyopita Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC, alimkaribisha Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake kwa chakula cha jioni na kujumuika pamoja na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao walikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia (World Bank Group) na International Monetary Fund (IMF) tarehe 12 - 17 Aprili 2016.
Kwenye ziara yake jijini Washington, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Afya (World Health Congress) na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani (International Commission on Financing Global Education Opportunity).


DSC_0447.JPG
Mhe. Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wao, Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Mama Marystella Masilingi


Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akibadiliashana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile (kushoto), Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu nyumbani kwa Mhe. Balozi , Tanzania House Bethesda, MD.