Punde baada ya kupokea habari ya kifo cha ghafla cha gwiji wa muziki wa Soukus Papa Wemba akiwa katika tamasha la muziki la Abidjan Ivory Coast , maelfu ya jamaa marafiki na mashabiki wake walianza kumiminika nyumbani kwake huko Kinshasa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Dadake Akita Helena na mamake Papa Wemba wamekuwa wakiwapokea waombolezaji nyumbani kwao Matonge.
Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba alifariki dunia baada ya kuzirai jukwaani
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,
Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.
Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa akitumbuiza jukwaani Abidjan.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo.
0 Comments