Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim.
Stori: Gladness Mallya, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM:  Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim amesema anakerwa na mastaa wanaodaiwa kuwa na tabia chafu zenye viashiria vya usagaji.

Shehe huyo aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kutafutwa na gazeti hili kufuatia kusambaa kwa picha mitandaoni zinazomuonesha mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na mwanamuziki Diana Exavery ‘Malaika’.
wema
Wema Sepetu
“Vitendo hivyo vinavyoashiria tabia za usagaji ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu, pia ni laana na havikubaliki kabisa katika imani yeyote, anayefanya vitendo hivyo anatakiwa kuachana navyo maana havimpendezi Mungu.
“Wasanii wote, wanapaswa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwao na si kuwapotosha,” alisema Shehe Alhadi.
wema-aunt
Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwa katika pozi tata.
Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Wema Sepetu kujianika akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na wanawake wenzake, alishawahi pia kuonekana katika pozi tata na mwigizaji Aunt Ezekiel.