Serikali ya jimbo la Nairobi imeanza kubomoa nyumba ambazo maafisa wanasema hazifai kuishi watu.
Shughuli hiyo inatekelezwa baada ya jumba moja la makazi la ghorofa sita kuporomoka Ijumaa wiki iliyopita na kuua watu 36.

jengo
Image captionWatu 36 walifariki baada ya jengo moja kuporomoka Ijumaa
Watu karibu 70 bado hawajulikani walipo.
Shughuli ya leo imelenga nyumba nane ambazo zimekuwa zikiishi watu karibu 600.
Nyumba ambazo zimepangiwa kubomolewa zimewekwa alama ukutani.
jengo
Image captionNyumba za kubomolewa zimewekwa alama
Watu waliagizwa wahame kutoka kwenye nyumba hizo wiki moja iliyopita.
Lakini kufikia leo asubuhi, baadhi ya watu walikuwa bado hawajahama.
Baadhi wamekuwa wakijaribio kuokoa mali yao mapema leo.
Baadhi ya wakazi wamelalamika kwamba hawana kwa kwenda.
Pesa
Image captionMwanamume huyu anasema hana pesa za kumsaidia kuhama. Anasema ana watoto watatu ambao wamo shuleni.