Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wanafunzi 2,000, wengi wao weusi kuimarisha juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi aliosema umebakia nchini humo.

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Howard mjini Washington, Bw Obama alisema hali ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika imeimarika sana tangu yeye atoke chuo kikuu mwaka 1983.
Image copyrightAFP
Image captionObama awaasa weusi Marekani
Lakini alisema kuchaguliwa kwake kwa rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika nchini humo hakujasaidia kupunguza ubaguzi wa rangi.
Bwana Obama alisema vijana hao wanapaswa kujivunia kuwa watu weusi lakini lazima wahakikishe kuwa wana mipango kambambe ya kuleta mabadiliko.