Kifo cha Muhammed Ali kimezua malumbano makali katika ulingo wa kisiasa miongoni mwa wagombea wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu, utakaofanyika mwezi Novemba nchini Marekani.
Katika risala zake za rambirambi mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, amesema kuwa Ali kwa hakika alikuwa Bingwa ambaye atakumbukwa na wengi.

Mwaka Jana, Ali alilaani wito uliotolewa na Bwana Trump, ya kuwazuia kabisa waislamu kuingia nchini Marekani.
Image copyrightREUTERS
Image captionAli alilaani wito uliotolewa na Bwana Trump, wa kuwazuia kabisa waislamu kuingia nchini Marekani.
Kwa upande wake mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Seneta Bernie Sanders, amemshutumu Bwana Trump na kumtaja kuwa mnafiki.
Naye Bi Hillary Clinton, amesema kuwa Bwana Trump, anafaa kuhukumiwa kwa matamshi yake anayotoa.
Bondia huyo alifariki siku ya Ijumaa huko Arizona, na alikuwa akiugua maradhi ya kusahau- sahau, kwa zaidi ya miaka thelathini.