Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 6, 2016

Viongozi kuanzisha kikosi cha Afrika Magharibi

Viongozi wa nchi za Magharibi mwa Afrika wamejadili mpango wa kuanzisha kikosi cha kupambana na wapiganaji wa Ki-Islamu katika kanda hiyo.
Wapiganaji wenye uhusiano na Al Qaeda wamefanya mashambulio nchini Mali, Ivory Coast na Burkina Faso, na kundi la Boko Haram, mara kadha, linashambulia maeneo ya Nigeria na nchi jirani.

Viongozi hao wanaokutana mji mkuu wa Senegal, Dakar, hawakutoa maelezo kuhusu mpango huo.
Pia wametaka uchaguzi ujao wa Gambia uwe huru, na askari wa usalama wasitumie nguvu nyingi dhidi ya raia.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP