Mwanamke mmoja mwandishi wa habari ameuawa kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Sagal Salaad Osman, ambaye alikuwa akifanya kazi na kituo cha serikali aliuawa na watu waliokuwa wamejihami na bastola.

Somalia ni moja ya nchi hatari zaidi duniani kwa waandishi wa habari, lakini kuuawa kwa waandishi wa habari wa kike si jambo la kawaida.
Hakuna kundi lililodai kutekeleza mauaji hayo, lakini huenda yametekelezwa na kundi la al Shabaab ambalo mara nyingi huwalenga waandishi wa habari.