Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, John Major, amewashutumu viongozi wanaoshinikiza Uingereza kujiondoa kutoka muungano wa mataifa ya Bara Ulaya, kwa kueneza udanganyifu na matamshi yenye uchafu.
Akiongea na BBC, Bwana Major aliwakabili wanaharakati hao wanaoendesha kampeini hiyo yenye uvumi, kwamba Uingereza huipa muungano wa EU Euro 350 Milioni kila wiki.

Bwana Major kila mmoja anafahamu kiwango ambacho Uingereza hutoa kama mchango wake kea EU huku akiongeza kuwa uvumi wa aina hiyo haufai kamwe.
Raia nchini Uingereza wanapiga kura hiyo ya maoni hatimaye mwezi huu wa Juni, ya iwapo isalie ndani ya muungano wa EU au ijiondoe.