Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 27, 2016

Wakimbizi 50,000 wa kisomali kuondoka Dadaab

Shirika la kuhudumia wakimbizi nchini Kenya limesema wakimbizi 50,000 wa kisomali wanaoishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab watarejea makwao kwa hiyari mwishoni mwa mwaka huu.

Shirika hilo limesema kila mkimbizi atakayerejea atapatiwa dola za marekani mia mbili pia msaada wa chakula na matibabu kwa kipindi cha mpaka miezi tisa.
Mamlaka za Kenya zimesema zinataka kufunga kambi, hasa ambazo zinawatunza wasomali.
Mamlaka hizo zimesema zitawahamisha wakimbizi wa kutoka Sudani Kusini na kuwapeleka kwenye Kambi nyingine.
Idadi ya wakimbizi kambini Dadaab huenda ikapungua mpaka kufikia watu laki moja na nusu mwishoni mwa mwaka.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP