Hamna dalili yoyote kuhusu kile kilichoipata ndege ya jeshi la wanahewa ya India, zaidi ya saa 24 baada ya kupaa kutoka Chennai ikielikea kisiwa cha Andaman.
Ndege hiyo aina ya AN-32 iliyotengenezewa nchini Urusi ilikuwa imebeba watu 29 wakiwemo raia.

Sasa waziri wa ulinzi nchini India Manohar Parrikar, anaongoza oparesheni kubwa ya kutafuta ndege hiyo baharini.
Ndege hiyo ilitoweka kutoka kwa mitambo ya rada dakika 15 baada ya kupaa angani.