Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 12, 2016

Sheria ya umiliki silaha tatizo Marekani

Kufuatia shambulio la mauaji ya Polisi watano nchini Marekani wiki iliyopita,mkuu wa katika jimbo la Texas amesema kuwa Polisi nchini Marekani wamesema sheria katika jimbo la Texas inayoruhusu raia kutembea na silaha ni moja ya mambo yanayowapa ugumu kudhibiti matukio ya mauaji ya kutumia silaha ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Mkuu wa polisi katika mji wa Dallas David Brown ameyasema hayo kufuatia shambulio la kutumia silaha lililosababisha vifo vya polisi watano wiki aliyopita, ambalo limefanywa na mtu aliyekuwa akimiliki silaha.
Katika kuhakikisha Marekani inakabiliana na vitendo hivyo vya mauaji ya kutumia silaha, Mjini Washngton Rais Barack Obama atakutana na makundi mbalimbali kuzungumzia njia tofauti za kuwapatia maafisa wa polisi mafunzo.
Leo anatarajiwa kuutembelea mji wa Dallas kushiriki mazishi ya waliouawa katika shambulio hilo.
Katika hatua nyingine, mgombea Urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump ambaye pia binafsi anajielezea kama '' Mgombea anayefuata Seria na amani'' ameaidi kuwalinda Wamarekani wote kwa kuwa mtu wa maamuzi magumu lakini bila ya upendeleo.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP