Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob akisalimiana na Mkuu wa Wialaya ya Ubungo Mhe. Humphrey Polepole alipokaribishwa katika Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam. Polepole amekaribishwa ili apate fursa ya kutambulishwa kwa Madiwani ambao kwa namna moja au nyingine atakuwa akifanya kazi nao kwa kuwa Wilaya yake imetokana na Manispaa hiyo.


Frank Shija,MAELEZO

Mchakato
wa kukamilisha taratibu za kuanza rasmi kwa shughuli za kiutendaji kwa
Ofisi za Mkuu wa wilaya na Manispaa ya Ubongo uhuko mbio kukamilika.

Kauli
hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni ambaye pia ni
Diwani wa Kata ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob wakati wa Kikao cha Baraza
la Madiwani leo jijini Dar es Salaam. Mhe. Jacob amesema kuwa
amearifiwa kuwa taratibu za kugawa rasilimali zimekamilika
kinachosubiriwa tu ni kukamilika kwa suala la upatikanaji wa majengo ya
Ofisi ambayo nayo yako mbioni kupatikana.

Jacob aliongeza kuwa
kukamilika kwa mchakato huo kutaongeza ufanisi katika uwajibikaji wa
kuwatumikia wananchi kwani Manispaa ya Kindondoni imekuwa ikitoa huduma
kwa idadi kubwa sana ya wananchi ila hali watendaji wake ni wachache
hivyo inawagharimu kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Naye Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Humprey Polepole akitoa salaamu zake baada ya
kukaribishwa katika Baraza hilo alisema kuwa wakati wowote shughuli za
kiutendaji katikaWilaya ya Ubungo zitakuwa zikitolewa katika Ofisi zake
kwani mchakato umekwisha kamilika.

“ Nifuraha yangu kuwa leo
nipo hapa na watumishi wenzangu wengine inawezekana tukawa Ofisi moja
katika wilaya yangu ya Ubungo, kwani nimearifiwa kuwa kila kitu
kimekamilika hadi mgawanyo wa watumishi” Alisema Polepole.

Aliongeza
kuwa anayo imani kuwa kazi iliyombele yake ni kuwatumikia wananchi wa
Ubungo kwa kuwaletea maendeleo hivyo ni vyema akapata ushirikianao kwa
wadau wote bila kujali itikadi zao.

Kuna namna mbili zipo
zinazitwa “Political Power “ na zile “Political Development”; nisema tu
mimi binafsi napenda tufanye Siasa ya Maendeleo kwa mustakabali wa
Ubungo yetu. Alisema.