Meneja
Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na timu ya StarTimes


na maveterani wa uwanja wa Mwembe Yanga – Temeke kabla ya mchezo wa kirafiki
uwanjani hapo. StarTimes iliweka kambi uwanjani hapo ikiwa ni uzinduzi wa
michuano ya ICC mwaka 2016 iliyokwishaanza kutimua vumbi Julai 22 wiki
iliyopita ambapo ilidhamiria kuonyesha mchuano mkali wa ‘Manchester Derby’
uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha
kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano
ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund
waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.
 Baadhi
ya wateja na mashabiki wa soka waliojitokeza kutazama mchezo wa
  ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini
Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa
kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya
Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa
magoli 4 - 1.


Mmoja
wa wateja waliofika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, akipata maelekezo
juu ya huduma za StarTimes kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wateja wa StarTimes na watanzania
kwa ujumla wameipongeza kampuni inayouza na kusambaza visimbuzi vya matangazo
ya dijitali, Starimes, kwa kuwaletea michuano ya kombe la mabingwa kimataifa au
ICC mwaka 2016 moja kwa moja kupitia chaneli yake ya ST WORLD FOOTBALL.

Hayo yalisemwa na wateja mbalimbali
waliohudhuria tamasha la uzinduzi wa michuano hiyo iliyoanza katika viwanja vya
Temeke, Mwembe Yanga.

Katika tamasha hilo StarTimes
walitinga viwanjani hapo na timu kamili ya wafanyakazi wake wa vitengo mbalimbali
ambapo pia walifunga luninga uwanjani ili kuonyesha moja kwa moja mtanange wa
watani wa jadi kutoka jiji la Manchester unaojulikana kama ‘Manchester Derby’
uliopangwa kufanyika jijini Beijing China lakini kutokana na hali ya hewa mbaya
ikabidi uahirishwe.

Akizungumza katika viwanja hivyo
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka alibainisha kuwa, “Siku ya
leo tumefika viwanjani hapa kwa lengo kubwa la kutaka kuwapa fursa wateja wetu
kujionea uhondo wa michuano ya ICC inayonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi
vyetu. Michuano hii inayofanyika katika nchi ya Marekani, Ulaya, Australia na
China inazishirikisha timu kubwa duniani kama vile Real Madrid, Barcelona,
Manchester United na City, Juventus, Chelsea, Liverpool na nyiginezo.”

“Michuano hiyo imekwishaanza tangu Ijumaa
ya wiki iliyoishia ambapo tumekwishashuhudia tayari timu kama Manchester
United, Borussia Dortmund, Celtic, Leicester City, Inter Milan na PSG
zimekwishatinga uwanjani. Siku ya leo tumekuja hapa kwa lengo la kuonyesha
Manchester Derby lakini tunasikikita kuwa mchezo huo umeahirishwa kutokana na
hali ya hewa mbaya kulikumba jiji la Beijing ambamo mchezo huo ulipangwa
kuchezwa. Lakini badala yake tunaonyesha mchezo wa marudio baina ya Manchester
United na Borussia Dortmund.” Aliongezea Bw. Kisaka

Meneja huyo wa Mauzo alimalizia kwa
kusema, “Ningependa kuchukua fursa hii kwa kuwashukuru wateja wetu kwa
kuendelea kufurahiamichuano hii mikubwa zaidi ambayo ni ya awali au maandalizi
kabla ya ligi kuu mbalimbali kuanza mwishoni mwa mwezi wa Agosti. 

StarTimes pia
tunaonyesha ligi hizo ambapo wateja watafurahia mechi zote za ligi za
Bundesliga na Serie A kupitia chaneli zetu za michezo za SPORT ARENA, SPORTS
FOCUS, WORLD FOOTBALL, SPORT LIFE NA SPORT PREMIUM na bila kusahau ligi za
Ufaransa na Ubelgiji kupita chaneli ya FOX SPORTS. 

Ili kufaidi michuano hii ya
ICC mwaka 2016 wateja itawabidi kulipia malipo kiduchu ya kifurushi cha Mambo
kwa shilingi 12,000/- tu na kuweza kutazama mechi zote moja kwa moja ambazo
zitarajiwa kuisha Agosti 13.”

Michuano ya ICC mwaka 2016
imekwishaanza Julai 22 ambapo mechi ya kwanza iliyofungua pazia ilikuwa ni kati
ya Machester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund iliibamiza United kwa
mabao 4 – 1. Michezo mingine iliyokwishachezwa ni pamoja na PSG kuitandika 3 -1
Inter Milan na Leicester City kuwashinda Celtic kwa mikwaju 6 – 5 ya penati
baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1 – 1 ndani ya dakika 90.



Siku ya leo Jumanne kutakuwa na
mechi nyingine ambapo mabingwa wa Italia, Juventus watashuka dimbani kuwakabili
timu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza katika mishale ya saa 7 mchana kwa muda
wa hapa nyumbani Tanzania kupitia chaneli ya WORLD FOOTBALL ndani ya ya
StarTimes pekee.