Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wake wa kazi alipozuru wilaya ya Same

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Same kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki


 Wananchi wakisikiliza kwa makini mkutano wa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro




Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki akitoa salamu kwa wajumbe wa kamati ya ulizni na usalama na salamu za kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadickalipotembelea Wilayani hapo

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadickakikagua mashine katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akipokea maelezo kuhusu mashine hizo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadickalipokagua mfereji wa Mshana

Na Mathias Canal, Kilimanjaro



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick amezuru katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same.

Sadick ametembelea kiwandani hapo akiwa ba dhamira ya kukifufua kiwanda
hicho ili kianze kufanya kazi ya izalishaji katika kiwango cha juu ili
kwenda sawia na kasi ya Maendeleo inayohitaji kwa wananchi wa eneo hilo
sambamba na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na wananchi kwenye
Mkutano wa hadhara alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho pia unapaswa
kutunza vyanzo vya maji lakini pia kuchemsha maji ya kunywa ili
kuepukana na Maradhi mbalimbali yatokanayo na unywaji wa maji yasiyo
safi na salama.

Katika sekta ya elimu amesema kuwa ni dhahiri
kuwa miundombinu ya shule inapaswa kuboreshwa ili waalimu wakae kwenye
vituo wanavyopangiwa na kuachana na tabia ya kuhamahama.

Rc Sadick amezungumzia pia mimba za utotoni ambapo amewataka wananchi
kuwaacha watoto wa kike waweze kusoma ili baadae wasiwe tegemezi
tofauti na ilivyo sasa anbapo wazazi wengi wanawaozesha wabinti wakiwa
na umri mdogo jambo ambalo ni kinyume kabisa na utaratibu wa ndoa kwa
mujibu wa sheria ya ndoa.

Kabla ya mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa
wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki
Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same
walifanya mazungumzo na Bodi ya uongozi wa Ushirika wa kiwanda hicho na
kuwataka waongeze juhudi kuhakikisha wakulima wa Tangawizi hawapati
hasara tena.

Rc Sadick ameutaka uongozi wa viwanda vidogo vidogo
SIDO ambao ndio wenye mitambo iliyofungwa kiwandani hapo kuboresha
mashine hizo ambazo kwa sasa zinatumia OIL chafu kuhamia kwenye umeme
ili kiwanda kiwe rafiki kwa mazingira pia.

Zao la Tangawizilinalimwa sana katika Kata hiyo ya Miyamba hivyo kufufuliwa kwa kiwanda
hicho kutaleta mapinduzi makubwa katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja
pamoja na kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.