Waziri wa habari Sudan Kusini amesema kuwa serikali haitajibu madai ya ripoti mpya inayodai kuwa viongozi wa nchi hiyo wananufaika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinayoendelea nchini humo.
Michael Maquei Lueth amesema kuwa serikali ina mambo mengi ya kusema kuhusu madai hayo lakini itafanya hivyo ikiwa itapatiwa rasmi taarifa za kina.
Ripoti iliyosimamiwa na muigizaji wa Hollywood na mwanakampeni George Clooney inadai kuwa Rais Salva Kiir,kiongozi wa upinzani Riek Machar na mkuu wa jeshi pamoja na familia zao wanafaida zinazofanana.
Inawaunganisha wasomi wa Sudan Kusini katika mchezo wa fedha unaojumuisha nyumba za kifahari, migodi ,mafuta na kampuni nyengine.
Vita hivyo vilivyoanza 2013 vimedhoofisha uchumi wa nchi
Image captionVita hivyo vilivyoanza 2013 vimedhoofisha uchumi wa nchi