Waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kaskazini mwa Tanzania Jumamosi wanaomba msaada ili kurejelea hali yao ya kawaida.
Watu 16 walifariki na wengine 250 kujeruhiwa kutokana na tetemeko hilo. Mamia wengine wamebaki bila makao.
Maafisa wa serikali katika eneo hilo bado wanaendelea kutathmini maafa yaliyosababishwa na tetemeko hilo la ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter.
Tetemeko hilo limetajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kukumba taifa hilo la Afrika Mashariki katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja.
Tetemeko hilo, ambalo kitovu chake kilikuwa kilomita takriban kilomita 44 kutoka mji wa Bukoba, mji mkuu wa mkoa wa Kagera kwa mujibu wa taasisi ya jiolojia ya Marekani.
Mitetemeko ilisikika maeneo ya Uganda, Kenya, Rwanda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mji huo, wenye wakazi 70,000, uliathirika pakubwa.Kufikia Jumatatu, waathiriwa walionekana kwenye vifusi vya majumba yao yaliyoporomoka wakijaribu kuokoa mali yao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliyetembelea mji wa Bukoba, ameagiza baraza la mji huo kufanya utathmini kubaini uharibifu uliotokea na kupendekeza jinsi serikali kuu inaweza kusaidia.
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais Edgar Chagwa Lungu ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko hilo.
Rais Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na mji wa Bukoba
Image captionKitovu cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na mji wa Bukoba
Rais wa nchi jirani ya Kenya Uhuru Kenyatta amezungumza kwa njia ya simu na Rais Magufuli kumpa pole zake na akaahidi kutoa usaidizi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Rais Kenyatta, Kenya itatoa msaada wa mabati, blanketi na magodoro.
Msaada huo utasafirishwa kwa ndege na jeshi la Kenya kesho Jumanne hadi maeneo yaliyoathiriwa nchini Tanzania, taarifa hiyo imesema.
Tetemeko