Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki
za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona
watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.


Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo ya siku tatu kwa
watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.


Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro
wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu
wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha
baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli
za utetezi.


Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya
Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea
kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010
ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya
wachimbaji wadogo wadogo wa madini.


Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili
ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili
wapatiwe ruzuku hiyo.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya maisha yao.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Washiriki wa Semina
Mwonekano kwenye semina
Picha ya pamoja