Urusi imesema kutakuwa na kusitishwa kwa muda kwa upigaji makombora katika mji wa Aleppo, nchini Syria kwa saa nane siku ya Alhamisi.
Afisa wa ngazi ya juu Sergei Rudskoi amesema majeshi ya serikali ya Urusi na Syria yatasitisha mashambulizi kuruhusu raia kuondoka katika mji huo na pia masuala ya tiba.

Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Umoja wa Ulaya wameilaani Urusi kwa kusababisha kile walichokiita mateso yasiyoelezeka.
Katika taarifa yao waliyoitoa baada ya mazungumzo ya Luxembourg, wamesema nguvu na ukubwa wa mashambulizi katika mji huo wa Syria ni wazi hayalingani na eneo hilo