Takriban wahamiaji 2,000 wameondolewa kwenye kambi ya ''Jungle'' mjini Calais nchini Ufaransa.
Takriban watu 7,000 wamekuwa wakiishi kwenye kambi hiyo katika mazingira magumu.

Wahamiaji walipanga mistari kwa amani kwa ajili ya kufuata taratibu za kuondoka kwenye kambi hiyo, lakini kumekuwa na maoni kuwa baadhi yao huenda wakakataa kuondoka kwenye kambi hiyo kwa kuwa wana nia ya kwenda Uingereza.
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Amber Rudd amesema takriban Watoto 200 kutoka kwenye kambi hiyo walipelekwa nchini Uingereza.
Rudd amesema Idadi hiyo inahusisha wasichana 60 waliokuwa hatarini kunyanyaswa kingono.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve amesema maafisa wamefikia lengo la kuwaondoa watu 2,000 kwa siku ya kwanza