Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 9, 2016

BREAKING NEWS..: VYAMA VITATU VYA SIASA VYAFUTIWA USAJILI WAKE LEO


Msajili vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi leo ametangaza kuvifutia usajili vyama vitatu vya siasa hapa nchini kwa kutumia kifungu cha 19 cha sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992, ambavyo ni vitatu, 1. Chama cha haki na ustawi (CHAUSTA)  kinachoongozwa na  James Mapalala, 2. Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT_Maendeleo)  kinachoongozwa na Peter Kuga Mziray, 3. Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na  Kasimu Bakari Ally.
Mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo unatokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika kuanzia juni 26 Mpaka julai 2016. 
Katika zoezi hilo, ilibainika kuwa vyama tajwa hapo juu vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria  ya vyama vya siasa na walipewa taarifa. Sababu za kufutwa vyama hivyo ni kutokuwa na ofisi ya Chama Tanzania bara na Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 10 d.
kutokuwa na wanachama Zanzibar kifungu cha 10 b, kushindwa kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya Chama  kifungu cha 14( 1) a,  kushindwa kuwasilisha hesabu zake za matumizi ya mwaka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mujibu wa sheria kifungu 14(1)b(1) ,   kushindwa kuwasilisha tamko la orodha za Mali za Chama kwa msajili vyama vya siasa  na mwisho kushindwa kutekeleza matakwa ya kifungu cha 15 (1) kwamba mapato yote ya fedha ya Chama yawekwe katika akaunti ya Chama.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP