Maeneo mengi Marekani yatasubiri vituo vifungwe- sana kati ya 19:00 EST (24:00 GMT - Saa tisa usiku Afrika Mashariki) na 20:00 EST (01:00 GMT - Saa kumi usiku Afrika Mashariki) - kuanza kupokea matokeo na makadirio ya matokeo katika majimbo mbalimbali.

Vituo vya kura vitafungwa katika jimbo lenye umuhimu mkubwa uchaguzini kutokana na wingi wa wajumbe, California (55), ambayo ni ngome ya Democratic, pamoja na Oregon (7), Washington (12), Idaho (4) na Hawaii (4).
Kwa kutegemea hali itakavyokuwa, mshindi anatarajiwa kutangazwa wakati huu.
Kwa kufuata desturi, atakayeshindwa anatarajiwa kutoa hotuba ya kukubali kushindwa muda mfupi baadaye.
Ilikuwa saa 00:00 EST (05:00 GMT) mwaka 2012 na 2008. Hata hivyo, mwaka 2004, John Kerry alisubiri hadi siku iliyofuata kukubali kushindwa.
Ukuzingatia madai ya Bw Trump kwamba kura zitaibwa, iwapo atashindwa, huenda akataka kura zihesabiwe tena au akatae kukubali kushindwa. Hilo likifanyika, hakuna ajuaye mshindi wa urais atatangazwa wakati gani.
Rais mteule atasubiri hadi 20 Januari mwakani kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani. Hili limeelezwa vyema kwenye katiba. Rais mteule ataweka mkono wake kwenye Biblia na kula kiapo saa sita mchana. Kuanzia hapo, atachukua udhibiti wa serikali.
Wataingia pia White House. Kawaida, rais anayeondoka na mkewe huandalia Rais anayeingia mamlakani na mkewe dhifa kabla ya sherehe ya kuapishwa. Saa sita baadaye, familia mpya huingia ikulu