Rais wa Guinea-Bissau Jose Mario Vaz amewafuta kazi mawazi wake wote.
Nchi ambayo ilionekana kuwa mfano wa maendeleo ya bara la Afrika, Guinea-Bissau sasa ni moja nchi maskini zaidi duniani, ambayo mara nyingi hukumbwa na misukosuko ya kisiasa na kijamii.

Mwaka 2015, mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani Raia Vaz, alimfuta kazi waziri wake mkuu na mwanachama mwenzake Domingos Simoes Pereira, kufuatia tofauti kati ya wawili hao ikiwemo kuteuliwa kwa mkuu mpya wa majeshi.
Bacijo Ja baadaye alichukua mahala pa Pereira lakini hilo halikumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo.
Hata hivyo Baciro Ja na baraza lake lote walifutwa kazi.