Rais mteule wa Marekani Donald Trump hatoanzisha uchunguzi mwengine kuhusu barua pepe za Hillary Clinton ili kumsaidia ''kujiuguza'',msemaji wake amesema.
Mshauri mkuu wa Trump, Kellyanne Conway amesema kuwa Trump hatotekeleza ahadi yake ya kumteua mwendesha mashtaka ili kumchunguza aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Hillary Clinton.

Bw. Trump alitishia kumfunga jela Bi Clinton na katika mikutano yake wafuasi wake walimuungan mkono kwa kusema ''mfunge jela!''
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani James Comey alimuondolea makosa bi Clinton.
Bi Conway alimwambia mtangazaji wa kipindi cha alfajiri cha MSNBC Joe Scarborough:Nadhani wakati rais mteule ambaye pia ni kiongozi wa chama chenu sasa ,Joe, anasema kabla hajaapishwa hapendelei kumfungulia mashtaka ,ni ujumbe mzito sana kwa wanachama.
''Na nadhani Hillary Clinton anafaa kujua kwamba raia wengi wa Marekani hawamuamini ,lakini Donald Trump anaweza kumsaidia kujiuguza,basi pengine kwamba hilo ni jambo zuri'',aliongezea.