WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, leo ameongoza wabunge kuuaga mwili wa Mbunge wa Dimani Zanzibar , Hafidh Ali Tahir mjini Dodoma.
Mbunge huyo ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa mjini Dodoma.
Baada ya marehemu Tahir kuagwa katika ofisi za Bunge, Waziri Mkuu na viongozi wengine akiwemo Spika wa Bunge, Job Ndugai walikwenda uwanja wa ndege kumuaga.
Mwili wa Mbunge huyo umesafirishwa kupelekwa Zanzibar kuzikwa.