Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. Kassim Majaliwa  anatarajiwa kutembelea Jiji la Arusha kuanzia kesho tarehe 01 hadi 03/12/2016 na
kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na watumishi wa Jiji, kukutana na
wafanyabiashara pamoja na kuzungumza na wananchi. 


Kwa mujibu wa Afisa habari wa Jiji la Arusha Nteghenjwa Hosseah, kesho tarehe 01/12/2016 Waziri mkuu MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea National Milling Company (NMC) na pia atakagua ujenzi wa barabara
ya Friends Corner - Muriet yenye urefu wa Km 7 inayojengwa kwa kiwango cha Lami
kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais
Tamisemi. 

Hosseah amesema siku ya tarehe 02/12/2016 Waziri Mkuu atakutana na kuzungumza na watumishi pamoja
walimu katika Ukumbi wa AICC Arusha na baadae atakutana na wafanyabiashara
katika Ukumbi huo.


"Katika nsiku ya tatu ya ziara yake Mhe Majaliwa  atatembelea na kukagua viwanda vya Lodhia
pamoja na Hans Paul vilivyoko mtaa wa Viwanda – Njiro na baadae atakutana na
wanachi wote kwenye Mkutano wa hadahara utakaofanyika kwenye uwanja wa Sheikh
Amri Abeid kuanzia saa nane mchana
.